Wabunge takribani wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, jana waliungana kupinga utaratibu uliowekwa na ofisi ya Bunge wa kujisajili mara mbili katika mfumo wa kielektroniki unaotambua alama za vidole.

Wabunge hao [isipokuwa mawaziri] waliunga mkono hoja ya kupinga utaratibu huo iliyowasilishwa na Mbunge wa Konde, Khatibu Said Haji (CUF).

Mbunge huyo alilitaka Bunge kutotumia utaratibu wa kujisajili mara mbili kwa mfumo huo (muda wa kuingia na kutoka) kwani wao pia hutumia muda mwingi wa mapumziko yao kufanya kazi za Bunge. Alisema hakuna haja ya kutumia utaratibu huo kwani wao sio wanafunzi, bali wajisajili mara moja pekee.

“Tatizo langu ni kitendo cha wabunge kutakiwa kusaini mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, wakati mwingine tunatoka hapa saa saba, wabunge tunashughulikia mambo mpaka saa 12, mbunge anatumia muda wake wa mapumziko na ule wa kuhudhuria kikao cha jioni,” alisema Mbunge huyo.

Hoja yake iliungwa mkono kwa kishindo na wabunge wote kwa kusimama na kumpigia makofi bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson aliwaeleza wabunge hao kuwa kutokana na namna ambavyo hoja hiyo imepokelewa, Bunge litaangalia upya suala hilo. Hata hivyo, aliwaeleza kuwa lengo la kujisajili mara mbili sio kuwafananisha na wanafunzi bali kujua mahudhurio yao.

Bodi Ya Wadhamini Young Africans Yaitega TFF
Jonas Tiboroha Kutimkia Mkoani Shinyanga