Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa nchini, Sisty Nyahonza amesema kuwa sheria inaruhusu kuchukua mkondo wake kwa Mbunge yoyote atakayezidisha kutumia gharama kubwa katika chaguzi mbalimbali, ambapo amesema gharama ya juu ni milioni 88

Ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha radio kilichopo jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa sheria hiyo imeanza mchakato mwaka 2006 na kukamilika 2010.

Aidha, gharama ya kuendesha kampeni za uchaguzi inatokana na ukubwa wa jimbo lenyewe lakini kuna kiwango maalumu ambacho taasisi imekipanga, ambacho cha chini kinaanzia milioni 33 huku kiwango cha juu ni milion 88.

”Kila jimbo lina kiwango chake, kama kiwango ambacho kimepangwa kikipita tunayo nguvu ya kuchunguza namna gani gharama kubwa imetumika ili muhusika achukuliwe hatua,”amesema Nyahoza

JPM amwaga mapesa mkutano wa CWT
LIVE: Kuagwa kwa Mashujaa waliopoteza maisha DRC