Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amewataka Wabunge kutojadili suala la Trilion 1.5 ndani ya bunge kutoka kwenye ripoti ya CAG, hadi kamati ya PAC itakapowasilisha ripoti yake.

Mhagama ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma mara baada ya Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kusimama na kuihoji Serikali kuhusu fedha hizo, ambazo ziliacha gumzo kubwa kwa umma na wanasiasa baada ya ripoti ya CAG kutolewa mapema mwa mwezi April mwaka huu.

Hata hivyo, Suala la upotevu wa Trilioni 1.5 kwenye ripoti ya CAG limeibua mjadala mkubwa kwa watu mbali mbali, huku wakiituhumu serikali kwa upotevu wake, licha ya Wizara ya Fedha kutoa mchanganuo wa taarifa hiyo na kuonesha kwamba hakuna upotevu wa fedha wa trilioni 1.5

 

UEFA yatoa adhabu kwa Gianluig Buffon
Rosa Ree afunguka kuhusu mistari ya Chemical ‘inayomkwaruza’