Nguli wa zamani wa Arsenal Emanuel Petit amewataka wachezaji wa timu hiyo kuacha mara moja kucheza soka kama watoto wadogo.

Kauli ya Petit imekuja baada ya Arsenal kuanza vibaya msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza ambapo katika mchezo dhidi ya Liverpool Arsenal ilikubali kipigo cha mabao 4-0.

Petit aliyewahi kuisaidia Arsenal kushinda ubingwa mwaka 1998 amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wamechangia kuifanya timu iwe na matokeo mabaya kwa kuwa wanacheza mpira kama watoto wadogo.

Kipigo cha mabao 4-o dhidi ya Liverpool kiliamsha hasira za mashabiki wengi wa Arsenal ambao wamekuwa wakienda uwanjani huku wakiwa na mabango yenye ujumbe unaomtaka kocha wa timu hiyo Arsene Wenger kujiuzuru.

”Wachezaji wanalipwa vizuri na kupewa motisha wanajivunia kucheza klabu kama Arsenal, kwanini haya yanatokea?” alihoji Emanuel Petit.

Mashabiki wa Arsenal na wachezaji wakubwa wa zamani wa timu hiyo wamekuwa na mitazamo tofauti huku baadhi wakimtupia lawama kocha wa timu hiyo na wengine wakiwalaumu wachezaji wa timu hiyo kwa kucheza chini ya kiwango.

Licha ya kupigiwa kelele tangu msimu uliopita kocha huyo wa zamani wa klaby ya Monaco ya Ufaransa amedai hana mpango wa kuondoka Arsenal.

 

 

 

Ibrahimovic atajwa katika kikosi cha Man Utd
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Septemba 5, 2017