Wachezaji wa klabu ya AS Vita Club wameahidiwa kiasi kikubwa cha pesa na Rais wao, mwanamama Bestine Kazadi, endapo wataifunga Al Ahly kesho Jumanne (Machi 16).

AS Vita Club watakua wenyeji wa mchezo huo wa mzunguuko wanne wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, hatua ya makundi, mjini Kinshasa, DR Congo.

Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 57 kupitia RTNC ya Congo amekiri kuwa wamewekeza katika kuhakikisha timu yao inafanya vizuri katika mchezo huo na kufika mbali kama malengo yao yalivyo kwa msimu huu 2020/21.

Kazadi amesema hawezi kueleza kiasi gani cha pesa watawapatia wachezaji kama motisha baada ya ushindi lakini ni pesa nyingi ambayo wataifurahia.

Bestine Kazadi

Katika mchezo wa mzunguuko watatu uliochezwa mjini Cairo, Misri mwanzoni mwa mwezi huu, AS Vita ililazimishwa sare ya 2-2, hali ambayo inatoa taswira ya ushindani mkubwa kuelekea mchezo wa kesho Jumanne (Machi 16).

AS Vita inashika nafasi pili kwenye msimamo wa Kundi A, kwa kumiliki alama 4 sawa na Al Ahly, lakini tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, inaziachanisha timu hiyo kwenye nafasi ya pili na tatu.

Simba SC inaendelea kuongoza msimamo wa kundi hilo kwa kufikisha alama 07, baada ya kuzifunga AS Vita na Al Ahly, huku akitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Al Merrikh.

Congo yaishtukia chanjo ya Corona
Museveni agoma Chanjo ya Corona 'bado-bado'