Baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wa Kombe la Shirikisho barani Afrika, wachezaji wa TP Mazembe wamejazwa noti na serikali ya  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia Waziri wa Michezo wa, Papy Nyango.

Waziri Nyango amekabidhi dola za kimarekani 5000 kwa kila mchezaji wa TP Mzembe kama hasante kwa serikali yake, kufuatia furaha aliyonayo kwa kuona klabu hiyo inavyoendelea kuipa heshima Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kitita hicho kutoka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia kwa Waziri huyo wa Michezo kinatajwa kuwa kama motisha kwa wachezaji hao na kuthamini mchango wa jasho lao mbele ya bendera ya Congo.

TP Mazembe waliifunga Super Sports Utd ya Afrika kusini mabao mawili kw amoja katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika mjini Lubumbashi majuma mawili yaliyopita, kabla ya kutoa sare ya bila kufungana katika mchezo wa mkondo wa pili uliochezwa Afrika kusini jumamosi.

Kiasi hicho cha fedha ni sawa na zaidi ya Shilingi milioni 11 za kitanzania.

Dr Nassoro Ally Matuzya afichua kinachomtesa Kamusoko
Ratiba ya kombe la Mapinduzi 2018 yaanikwa hadharani

Comments

comments