Imebainika kuwa wachezaji wa Arsenal wamesafiri kwa zaidi ya Maili 48,869 angani walikapokua wanarejea kwenye makao makuu ya klabu hiyo kaskazini mwa jijini London, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa mwishoni juma hili dhidi ya Man Utd.

Asilimia kubwa ya wachezaji wa Arsenal walitapakaa kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya kucheza michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, kwa kipindi cha juma moja na nusu.

Uchunguzi uliofanywa na kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini England, umebaini mshambuliaji Alexis Sanchez amesafiri umbali wa Maili 14,416 angani akitokea nchini kwao Chile baada ya kumaliza majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa katika mchezo dhidi ya Uruguay hapo jana.

Malinda mlango namba mbili wa kikosi cha Arsene Wenger, David Ospina, naye amekadiriwa kusafiri umbali wa Maili 14,416 akitokea nchini kwao Colombia.

Alex Iwobi amesafiri Maili 6,424 akitokea Nigeria, Mohamed Elneny (Maili 4,208 akitokea Misri) pamoja na Shkodran Mustafi (Maili 2,428 akitokea Ujerumani), tofauti na Theo Walcott ambaye alibaki nyumbani England akiitumikia The Three Lion.

Beki wa pembani Hector Bellerin amesafiri kutoka nyumbani kwao Hispania, pasi na kucheza mchezo wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 kwa umbali wa Maili 1,964.

Hata hivyo wachezaji wengine wa Arsenal walibaki jijini London wakiendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Man Utd kutokana sababu mbalimbalia mbazo ziliwanyima nafasi ya kuitwa katika timu zao za taifa.

Mlinda mlango namba moja Petr Cech, hakurudi nyumbani Jamuhuri ya Czech kufuatia maamuzi ya kustaafu kuichezea timu yake ya taifa, Francis Coquelin, Mesut Ozil, Gabriel Paulista, Alex Oxlade-Chamberlain, Carl Jenkinson pamoja na Kieran Gibbs hawakuitwa kwenye vikosi vyao.

Image result for Man Utd Vs Arsenal Players 19 nov 2016 - Sky Sports

Kwa upande wa Man Utd wachezaji wao wamesafiri kwa umbali wa Maili 30,883 angani wakati wa michezo ya kimaitaifa iliyozihusu timu zao za taifa.

Mlinda mlango chaguo la pili Sergio Romero amevunja rekodi ya kuwa mchezaji aliyesafiri kwa umbali mrefu zaidi tofauti na wengine katika kikosi cha Jose Mourinho.

Mlinda mlango huyo amesafiri kwa umbali wa Maili 14,338 angani akitokea nyumbani kwao Argentina, huku kiungo mshambuliaji wa Armenia Henrikh Mkhitaryan akisafiri umbali wa Maili 4,694.

Mlinda mlango chaguo la kwanza David de Gea pamoja na viungo Juan Mata na Ander Herrera wote wamesafiri kwa umbali wa Maili 2,297 wakitokea nchini kwao Hispania, Matteo Darmian (Maili 756 akitokea Italia) na Memphis Depay (Maili 457 akitokea Uholanzi).

Waliobaki kikosini kwa sababu za kutojukumika na timu zao za taifa ni Marcus Rojo, Phil Jones, Anthony Martial, Michael Carrick, Ashley Young, Morgan Schneiderlin na Timothy Fosu-Mensah huku Zlatan Ibrahimovic na Bastian Schweinsteiger wakiwa wamestaafu kuzitumikia timu za mataifa yao.

Wengine ni Eric Bailly, Luke Shaw, Antonio Valencia, Marouane Fellaini pamoja na Chris Smalling ambapo wote kwa pamoja hawakuitwa kwenye timu zao za taifa, kutokana na sababu za kuwa majeruhi.

Tathmini ya umbali za safari kwa wachezaji wa vikosi vya Arsenal na Man Utd, imefanyika kwa lengo la kupima uzito wa mchezo wa mwishoni mwa juma hili.

Juanfran: Antoine Griezmann Atacheza Dhidi Ya Real Madrid
Mbarawa azindua bodi mpya TRL