Ni baada ya ndege yao kutumia uwanja wa kimataifa wa Orly, jijini Paris kama kituo, ilipokuwa ikitokea Morocco ikielekea Algeria, walipochuana na Niger mapema mwezi huu, katika kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2022.

Bilal Ahmed Hassan, Nasradine Abdi na Hilmi Aboubaker, waligoma kabisa kuendelea na safari yao mara tu baada ya kutua Paris, wakidai kuwa usalama wao ni mdogo nchini kwao Djibouti.

Djibouti, taifa dogo lililopo Pembe ya Afrika, linaongozwa kwa zaidi ya miaka 20 sasa na Dikteta Ismaïl Omar Guelleh.

Mara baada ya ndege iliyokuwa ikiwabeba wachezaji wa Djibouti kuondoka Paris, Bilal, Nasradine na Hilmi walipokelewa na Ofisi za uhamiaji jijini Paris.

Wote wamepewa nyumba na kibali cha makazi cha muda wa miezi 6 Maji, umeme na gesi ni kwa gharama za serikali…

Kila mwezi, watapewa posho ya Euro 440, sawa na shilingi za Tanzania 1,232,000.

Baada ya miezi 6, endapo serikali ya Ufaransa itajiridhisha kuwa usalama wao ni mdogo nchini kwao, watapewa kibali cha kudumu.

Djibouti ni Koloni la zamani la Ufaransa na lugha rasmi nchini humo ni Kiarabu na Kifaransa.

Hitimana aomba msamaha Mtibwa Sugar
Azim Dewji: Manara anashangaza, angegombea ubunge