Saa chache baada ya kutua jijini Dar es salaam wakitokea Songea mkoani Ruvuma, Wachezaji wa Young Africans walifika Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kuaga mwili wa Baba Mzazi wa Beki wa kulia wa klabu hiyo Paul Godfrey ‘Boxer’.

Mzee Godfrey Nyang’anya alifikwa na umauti siku moja baada ya kikosi cha Young Africans kuwasili mjini Ruvuma mkoani Songea, kwa ajili ya mchezo wa Mzunguuko wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC FC.

Kwa majonzi makubwa wachezaji wa Young Africans walifika Hospitali ya Temeke ikiwa ni sehemu ya kumfariji mchezaji mwenzao, ambaye alilazimika kurejea jijini Dar es salaam.

Mbali na Wachezaji, pia baadhi ya viongozi wa Young Africans walijumuika na Mfiwa hispotalini hapo.

Young Africans jana Jumanne (Oktoba 19), ilicheza dhidi ya KMC FC mjini Songea mkoani Ruvuma katika Uwanja wa Majimaji, na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mulamula: Mazingira ya uwekezaji ni salama
Aliyekufa aibukia kituo cha polisi