Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Mohamed Nabi amesema, amewapiga marufuku wachezaji wake kuendelea na furaha ya Ubingwa, baada ya kukamilisha sherehe usiku wa kuamkia jana Jumatatu (Juni 27).

Young Africans ilisheherekea Ubingwa wa Tanzania Bara kwa mbwembwe na vifijo Jumapili (Juni 26), kwa kusindikizwa na Mashabiki wake baada ya kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere ikitokea Mbeya ilipokua na mchezo dhidi ya Mbeya City FC, uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Nabi amesema aliwataka wachezaji wake kusitisha furaha ya kutwaa ubingwa, na kufikiria zaidi mchezo wa kesho Jumatano (Juni 29) dhidi ya Mtibwa Sugar, ambao utaunguruma Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

“Niliwapiga marufuku wachezaji wote kuendelea na sherehe za ubingwa, nimewaambia wafikirie sana mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar, tunapaswa kutambua kazi haijaisha kwa msimu huu, furaha inapaswa kuendelea lakini sio katika kipindi hiki ambacho majukumu yametukaba.”

“Itapendeza zaidi kuendelea kupambana kuliko furaha ya Ubingwa, kila mmoja nilimwambia hili na tumeelewana, niliwaambia waachieni mashabiki waendeleze furaha za ubingwa wetu.” Amesema Kocha Nabi.

Vijana wanolewa Ujuzi Tepe
Kocha Nabi aihofia Mtibwa Sugar Kwa Mkapa