Wachimbaji 6 wa madini hawajulikani kama wapo hai ama wamefariki baada ya kufukiwa na maporomoko ya udongo katika mgodi wa Copper Hill Gold Mine uliopo katika eneo la Migori nchini Kenya.

Mwenyekiti wa eneo hilo, Christopher Okello amesema kuwa wachimbaji hao walikuwa katika taratibu za kutoka machimboni wakati ukuta wa udongo ulipoanguka

Waliofukiwa katika machimbo hayo ni pamoja na Ominde Achineg (48), Ochieng Mwalimu (37), Atineo Abongo (26) Odhiambo Opiyo (28), Isiah Otwera (27) na Pascal Ochieng (30).

Aidha, taratibu za kuwaokoa zinaendelea lakini kutokana na ugumu wa miamba waokoaji wanapata ugumu kufanya haraka na hivyo kuagiza gari la uchimbaji miamba kwenda kusaidia

Hata hivyo, haijafahamika mara moja sababu za ukuta huo kuanguka ingawa, Okello amesema kuwa inaweza kuwa imesababishwa na mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo.

 

Video: NBS yafunguka kuhusu mfumuko wa bei
Video: Mwanzo mwisho spika alivyombana Mwijage, Agizo la JPM lawasha moto Iringa