Wizara ya Nishati na Madini, kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) inatarajia kuanza kutoa Ruzuku ya  jumla ya Shilingi Bilioni 7.481 kwa Wachimbaji Madini Wadogo 59 ambapo kiwango cha juu cha Ruzuku kwa Kikundi/Mtu binafsi kikiwa ni  Shilingi Milioni 210.

Aidha, zoezi hilo linatarajiwa kuanza kufanyika siku ya Jumatatu , tarehe 16  Januari 2017, Mjini Mpanda mkoani Katavi, Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Fedha za Ruzuku kwa kila Mnufaika, zitatumika kununua vifaa vya kuchimbia au kuchenjulia madini ambapo kabla ya kukabidhiwa vifaa hivyo, wanufaika hao watapata mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya ruzuku yatakayotolewa na Wizara ya Nishati na Madini tarehe 15 Januari, 2017 Mjini Mpanda.

Hata hivyo, miradi 59 inatarajiwa kupata ruzuku hiyo, ndiyo iliyoshinda kati ya miradi 592 ya uchimbaji madini mdogo iliyokuwa kwenye ushindani,Waombaji wengine ambao maombi yao hayakushinda watajulishwa kwa Barua.

Wizara ya Nishati na Madini ilianza mchujo wa kuwapata Washindi tangu Mwezi Julai 2016, kwa kuwashirikisha , Viongozi wa Wachimbaji Madini Wadogo wa mikoani (REMA’s),Viongozi wa Kitaifa  (FEMATA) pamoja na Viongozi wa Wachimbaji Madini Wanawake (TAWOMA).

Majaliwa: Tutaendeleza uhusiano wetu na china
#HapoKale