Watu wenye asili ya China duniani wanaadhimisha mwaka mpya wa Kichina, maarufu kama mwaka wa Nyani (New Year of the Monkey).

Wachina wanaadhimisha mwaka huo leo ikiwa Nyani ni mmoja kati ya wanyama kumi na mbili wanaoheshimiwa katika imani yao na hutumika kwenye alama za Kichina kwa ajili ya Utabiri wa mambo mbalimbali.

Maelfu ya wananchi wa China wamekusanyika jijini Beijing kuadhimisha sherehe hizo huku wakipiga mafataki na kucheza ngoma za asili zinazoambatana na maonesho ya michezo mbalimbali ukiwemo mchezo maarufu wa ‘Dragon’.

Dragon

Sherehe hizo pia zimeadhimishwa kwa shangwe kubwa mjini Yokohama ambapo wao wamesherehekea kwa kuhesabu muda.

Jiji la London linatajwa kuwa jiji litakaloshuhudia sherehe kubwa zaidi za mwaka huo mpya nje ya China.

Mawaziri wa Zamani waanza kutumikia adhabu ya kusafisha Hospitali
Polisi amtaja aliyemuua 2 Pac Shakur, adai alitumwa na P-Diddy