Raia wanne wa China wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuendesha kiwanda cha kutengeneza mifuko ikiwemo ya plastiki kinyume na sheria huku kiwanda hicho kikitozwa faina ya shilingi Milioni 7 kwa makosa ya kisheria.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde wakati wa ziara yake jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa raia hao wa kigeni wamekiuka taratibu na sheria za uendeshaji kiwanda kilichopo kwenye makazi ya watu na kuagiza kifungwe kwa muda ili kupisha uchunguzi wa usajili wake.

Amesema serikali inawapenda wawekezaji kwenye sekta ya viwanda na inataka waje kwa wingi kuwekeza nchini lakini ni lazima nao wafuate sheria za nchi katika uwekezaji wao ili kila upande uweze kufaidika na uwekezaji huo.

 

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 19, 2017
Video: Dkt. Shika kutumiwa mabilioni yake kutoka Urusi, ayalipia Bima