Klabu ya Southampton ya nchini England, huenda ikanunuliwa na na kampuni ya kibiashara kutoka China.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa, mmiliki wa sasa wa klabu hiyo Katharina Liebherr anafanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya kichina na tayari ameshatangaza dau la Pauni milioni 200.

Liebherr alirithi umiliki wa klabu ya Southampton kutoka kwa baba yake mzazi aitwae Markus, ambaye alifanikisha kuinusuru na janga la kufikilisa mwaka 2009.

Tayari klabu za West Brom, Aston Villa, Wolves pamoja na Birmingham zimeshanunuliwa na wafanyabiashara kutoka nchini China huku klabu ya Hull City ikiwa mbioni kumilikiwa na muwekezaji kutoka Hong Kong.

Meneja wa klabu ya Southamprton Claude Puel, tayari ameshatoa baraka za kuwa chini ya muwekezaji mpya na ameahidi kufanya nae kazi bila hiyana.

Meneja huyo kutoka nchini Ufaransa, alitoa maelezo hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliohusu mchezo wa Europa League ambao utawakutanisha na Inter Milan usiku wa leo.

Video: Machinga watua Bungeni Dodoma, Serikali yatoa majibu
Mamadou Sakho Akaribia Mlango Wa Kutokea Anfield