Watu wasiofahamika ambao walikuwa ni sehemu ya wandamanaji wamelivamia jengo la Bunge la Libya na kuchoma sehemu ya majengo, wakilalamikia kuzorota kwa hali ya maisha na mkwamo wa kisiasa.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo mbalimbali vya Habari, vimesema waandamanaji hao walifanikiwa kupenya ndani ya jengo hilo na kufanya vitendo vya uharibifu, huku vijana wenye hasira wakichoma matairi katika eneo hilo la Bunge lililopo mji wa mashariki wa Tobruk Juni mosi, 2022.

Bunge la Libya, kama Baraza la Wawakilishi limekuwa na makao yake katika mjini wa Tobruk, uliopo mashariki mwa mji mkuu nchi hiyo Tripoli, tangu mfarakano wa mashariki-magharibi wa mwaka 2014 kufuatia uasi uliomwondoa madarakani Moamer Kadhafi miaka mitatu iliyopita.

Baraza pinzani, linalojulikana rasmi kama Baraza Kuu la Jimbo liko jijini Tripoli huku picha zikionesha kuwa muandamanaji aliyekuwa akiendesha tingatinga alifanikiwa kupenya sehemu ya lango, na kuwaruhusu waandamanaji wengine kuingia kwa urahisi zaidi, na magari ya viongozi yakichomwa moto.

Libya imestahimili siku kadhaa za kukosa kwa nguvu, kutokana na kuzingirwa kwa vituo kadhaa vya mafuta dhidi ya hali ya migogoro ya kisiasa na Serikali mbili zimekuwa zikigombea madaraka kwa miezi kadhaa.

Kufuatia tukio hilo, Mbunge Balkheir Alshaab amesema ni lazima wabunge wenzake watambue kushindwa kwao na pia wajitahidi kusoma nyakati ili kujiondoa mara moja kwenye ulingo wa kisiasa.

“Natoa wito kwa wabunge wenzangu pamoja na wajumbe wa Baraza Kuu la Serikali kujiuzulu kwa pamoja ili kuheshimu matakwa ya watu wa Libya na kulinda utulivu wa Libya,” mbunge Ziad Dgheim, alinukuliwa na idhaa ya Libya Al-Ahrar siku ya Ijumaa. .

Uchaguzi wa Rais na Wabunge, uliopangwa kufanyika Desemba mwaka jana, ulikusudiwa kuhitimisha mchakato wa amani unaoongozwa na Umoja wa Mataifa kufuatia kumalizika kwa duru kuu ya mwisho ya ghasia mwaka 2020.

Lakini kura hiyo, haikufanyika kwa sababu ya wagombea kadhaa kuweka utata na kutokubaliana kwa kina juu ya misingi ya kisheria wa uchaguzi kati ya vituo pinzani vya nguvu mashariki na magharibi.

Umoja wa Mataifa ulisema mazungumzo kati ya taasisi hasimu za Libya yenye lengo la kuvunja mkwamo yameshindwa kutatua tofauti kuu, huku Spika wa Bunge Aguila Saleh na rais wa Baraza Kuu la Nchi Khaled al-Mishri wakikutana katika Umoja wa Mataifa huko Geneva kwa siku tatu za mazungumzo kujadili rasimu ya mfumo wa katiba wa uchaguzi.

Serikali yataka huduma bora kwa wananchi
Utalii wa baridi watakiwa Njombe