Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko ameagiza watalaamu wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, ambao wamekuwa wakisababisha kupatikana kwa hoja za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG wachukuliwe hatua.

Amesema hayo leo Juni 14, 2021 katika kikao kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga, kilichokuwa na ajenda moja ya kujadili hoja zilizotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG, katika mwaka wa fedha 2019-2020.

“Kwa hoja ambazo zimetolewa na CAG katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, nilivyoziona zinatokana na uzembe kabisa, haiwezekani mtu anakaa na fedha za mapato mfukoni hata mwezi mmoja na kutozipeleka benki,” amesema Mboneko.

“Ifike mahala watu ambao wanatusababishia hoja hizi za CAG wachukuliwe hatua, kwa sababu baadhi ya hoja zinajirudia rudia kila mwaka hili hatuwezi kulivumilia,” ameongeza Mboneko

Mkuu wa Twitter aweka bendera ya Nigeria mtandaoni
Bilioni 1.5 zatengwa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa