Jeshi la Polisi nchini Rwanda limesema kuwa linawshikilia wachungaji 6 na viongozi wa makanisa kutoka katika makanisa yaliyofungwa kwa amri ya serikali ya nchini humo.

Wiki iliyopita Serikali ya nchi hiyo iliamrisha kufungwa kwa makanisa zaidi ya 700 kwa madai ya kutotimiza kanuni za ujenzi wa makanisa yao.

Aidha, Wachungaji hao wamekamatwa baada ya rais Paul Kagame kuyatuhumu hadharani kuwa makanisa hayo mengi hayana sifa za kuwa makanisa.

Hata hivyo, Rwanda inajadili sheria mpya ambayo itahusu mashirika yenye misingi ya imani na dini yanayo endeshwa na wahubiri kuwa wahubiri hao lazima wawe na shahada za elimu ya theolojia.

Waziri Dkt. Mwakyembe kuipa nguvu Yanga
Afrika kusini waandamana kushinikiza haki kifo cha Mtanzania aliyeuawa kikatili