Wadau  wa elimu wa manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wamekuwa na mtazamo tofauti  juu ya agizo la Rais Magufuli kufuta michango kwa wanafunziwa shule za msingi na sekondari, huku miundombinu ya shule nyingi mkoani humo ikiwa si ya kuridhisha jambo lililosababisha wanafunzi zaidi ya 1553 kukosa nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu.

Wadau hao wamesema kuwa tamko la Rais halikuzingatia Jografia ya maeneo ya pembezoni  mwa nchi kama vile mkoa wa Rukwa. Walidai kuwa ili kuinua hadhi ya elimu ambayo imekuwa nyuma tangu uhuru, ushiriki wa wananchi hauepukiki.

“Ni kweli serikali imetoa zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika manispaa yetu, lakini fedha hizi ni tone ukilinganisha na matatizo tuliyo nayo. Haziwezi kutatua kila changamoto tulizonazo. Hivyo basi michango ya wadau na wazazi haiepukiki,” alisema Zeno Nkoswe mdau wa elimu wakati wa mkutano wa wadau wa elimu manispaa ya Sumbawanga.

Shule nyingi za msingi na sekondari  mkoani Rukwa zimekuwa zikikabiliwa na changamoto mbalimbali huku zingine zikikosa miundombinu ya  vyumba vya madarasa  uchakavu wa  majengo pamoja na uhaba wa matundu ya vyoo.

Azam FC yaanza kuivutia kasi Mtibwa Sugar
Muuguzi awaingiza chaka madaktari, wafanya upasuaji wa ubongo kwa mtu asiyehitaji upasuaji