Serikali, imesema imependezwa na utayari, ushiriki na uchangiaji wa Wananchi na wadau mbalimbali waliojitokeza na kusaidia watoto kupata huduma ya upasuaji wa moyo kupitia mchezo wa riadha, huku Kampuni ya DataVision Internatinal ikishiriki zoezi hilo kikamilifu.

Hayo, yamebainishwa hii leo Agosti 14, 2022 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye hitimisho la mbio zilizoandaliwa na CRDB Marathon na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema, ushiriki huo umeonesha namna jamii ilivyoshikamana na kutambua watu walio na uhitaji wa matibabu na hivyo kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na kuwawezesha kuondokana na maradhi mbalimbali hasa ugonjwa wa moyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.

Kenya: Madai ya udanganyifu wa matokeo yazidi kutawala

“Niwapongeze wananchi na wadau waliojitokeza katika zoezi hili na sisi kama Viongozi wa Serikali hatuna budi kuwashukuru kwa hili ni jambo la kuungwa mkono kuwasaidia watoto kuweza kupata huduma ya upasuaji wa moyo,” amesema Makamu wa Rais.

Awali wakihojiwa na Dar 24, Meneja wa Oparesheni wa DataVision Internatinal, Vedigrace Nkini amesema amefurahi kushiriki zoezi hilo kwani yeye kama mama anatambua umuhimu wa kuwasaidia na kuchangia akina mama wenye matatizo ya ujauzito hatarishi na watoto wenye matatizo ya moyo.

Amesema “Naushukuru uongozi wa DataVision International na wana DataVision wenzangu, na katika marathon hii nimeshiriki kwa niaba ya wamama ambao wana matatizo wakati wa kujifungua na hata kwa watoto ambao wana changamoto ya magonjwa ya moyo.

Bi. Nkini ameongeza kuwa, kwa kutambua umuhimu wa watoto yeye kama mama ameona ni vyema kushiriki zoezi hilo ili kuweza kuwasaidia kuondokana na maradhi yanayowakabili hasa wenye matatizo ya moyo.

Kikwete akishangaa cheo chake, adai hajui jukumu lake
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 14, 2022