Wadau wa haki za watoto hasa wenye umri wa zaidi ya miaka 10,  wametakiwa kujadili na kuweka mpango mzuri wa kuwalinda dhidi ya  vitendo vya udhalilishaji na ukatili.

Hatua hiyo, imetokana na takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Afisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, zinaonesha watoto 1,173 waliathirika na vitendo vya udhalilishaji na ukatili kwa mwaka 2022.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, jumla ya matukio 883 (asilimia 75%) ambayo yaliripotiwa ni kwa watoto hao wenye umri kati ya miaka 11 hadi 17 ambapo TAMWA-ZNZ imeona upo umuhimu wa kutafuta muafaka juu ya tatizo hilo.

Utafiti wa kihabari wa TAMWA ZNZ, uligundua kuwa matatizo ya matumizi mabaya ya kimtandao kwa vijana wa kiume yanachochea kutaka kujihusisha na masuala ya ubakaji, wakati tamaa kwa watoto wa kike nayo ikichangia. 

Azaki waaswa kushirikiana na Halmashauri, jamii
Morocco, Iraq wafungua ubalozi baada ya miaka 18