Klabu hii makazi yake ni Mbarali Mbeya na inashiriki Ligi daraja la kwanza na nzuri zaidi kwenye msimamo wa Ligi inashika nafasi ya Pili ikiwa na alama 39 nyuma ya Dodoma FC, yenye alama kama hizo 39, tofauti yao Ni magoli ya kufanga na kufungwa.

Klabu ya Ihefu yenyewe inamiliki Uwanja wake binafsi wenye jina la Highland Estates Stadium ilioko huko huko Mbarali, Mbeya.

Na tamu zaidi utakumbuka msimu wa Mwaka 2017/18 timu hii ilicheza na Young Africans mchezo wa Kombe La Shirikisho (ASFC) raundi ya tatu na mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo ilikuwa 1-1, almanusla Young Africans wang’olewe.

Kwani mpaka dakika 80 IHEFU ilikuwa mbele kwa bao moja. Timu hizo zilikwenda penati ambapo Young Africans ilishinda kwa mbinde mabao 4-3.

Klabu ya Ihefu inamiliki Basi lenye thamani ya shilingi milioni 350, ikiwa ni ahadi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Mkoni Mbeya Haroon Pir Mohamed.

Basi hilo ni gharama zaidi kuliko mabasi ya Azam FC, Simba SC na Young Africans. Mabasi yanayotumika na timu hizo ni Yutong F11 yenye thamani ya shilingi milioni 250 kila moja.

Van Persie: Van Gaal alinichapa kofi 2014
Aristica Cioaba kukosa ligi kuu, kombe la shirikisho

Comments

comments