Fainali za 31 za mataifa ya Afrika zimepangwa kuanza rasmi mwishoni mwa juma hili katika nchi ya Gabon na mataifa 16 ya bara hilo yapo katika hatua za mwisho za maandalizi.

Fainali za mwaka 2017 zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na utayari wa timu shiriki, ikiwa ni sambamba na mabingwa kihistoria, timu ya taifa ya Misri.

Dar24.com inalazimika kukumbusha mabingwa ambao waliwahi kupatikana kwa miaka ya nyuma wakiongozwa na mafarao ambao watakua wakishiriki kwa mara ya 23 katika fainali za mwaka huu 2017.

Orodha ya mabingwa wa Afrika tangu fainali hizo zilipoanza rasmi mweaka 157.

1957 – Misri (Sudan), 1959 – Misri (Misri), 1962 – Ethiopia (Ethiopia), 1963 – Ghana (Ghana), 1965 – Ghana (Tunisia), 1968 – Congo-Kinshasa (Ethiopia), 1970 – Sudan (Sudan), 1972 – Congo (Cameroon), 1974 – Zaire (Misri) na 1976 – Morocco (Ethiopia).

1978 – Ghana (Ghana 1980 – Nigeria (Nigeria 1982 – Ghana (Libya) 1984 – Cameroon (Ivory Coast), 1986 – Misri (Misri), 1988 – Cameroon (Morocco), 1990 – Algeria (Algeria), 1992 – Ivory Coast (Senegal), 1994 – Nigeria (Tunisia), 1996 – Africa Kusini (Africa Kusini) na 1998 – Misri (Burkina Faso).

2000 – Cameroon (Ghana na  Nigeria), 2002 – Cameroon (Mali), 2004 – Tunisia (Tunisia), 2006 – Misri (Misri), 2008 – Misri (Ghana), 2010 – Misri (Angola), 2012 – Zambia (Equatorial Guinea na  Gabon co-hosts), 2013 – Nigeria (Africa Kusini) na 2015 – Ivory Coast (Equatorial Guinea).

Muhimu: Nchi zilizowekwa katika mabano zilikua mwenyeji wa michuano ya AFCON kwa mwaka husika.

Orodha kwa idadi ya nchi zilivyowahi kuchukua ubingwa wa Afrika.

Misri   7 (1957, 1959*, 1986*, 1998, 2006*, 2008, 2010)

Ghana      4 (1963*, 1965, 1978*, 1982)

Cameroon 4 (1984, 1988, 2000, 2002)

Nigeria     3 (1980*, 1994, 2013)

Ivory Coast       2 (1992, 2015)

DR Congo 2 (1968, 1974)

Zambia     1 (2012)

Tunisia     1 (2004*)

Sudan       1 (1970*)

Algeria     1 (1990*)

Morocco   1 (1976)

Ethiopia   1 (1962*)

Africa Kusini    1 (1996*)

Congo      1 (1972)

Timu shiriki kwa mwaka huu 2017 ni Gabon, Ivory Coast, Ghana , Algeria, Tunisia, Mali, Burkina Faso, DR Congo, Cameroon, Senegal, Morocco, Misri, Togo, Uganda, Zimbabwe na Guinea-Bissau.

Rais Shein awapa ‘neno’ wanaofikiri ataondolewa madarakani na UN
Rais wa zamani wa Iran afariki dunia