Niliketi sebuleni kwangi nikiangalia sinema ya jinsi VIBAKA wanavyokwapua watu. katika kitongoji cha SOWETO nikatamani niwageuza vijana hawa wacheze mpira ili WAPORE pointi badala ya kupora watu..ANASIMULIA .James Sofasonke Mpanza au the Father of South West Town (SOWETO) na anamalizia kwa kusema hii ndiyo asili ya Jina PIRATES..jina Orlando (1937) ni asili ya Kitongoji ambacho timu hii iliasisiwa na kupewa jina kamili la Orlando Pirates (awali kabisa iliitwa Orlando Boys (1932)

Sababu Nyingine ya Kuiita Pirates ni kwamba Muasisi wa Timu hii ndiye aliyeongoza UVAMIZI NA UPORAJI wa kuupora mji wa SOWETO na ndio maana anaitwa The Father of SOWETO

Kwa Afrika Kusini Ukizungumza Orlando Pirate ni kama unaizungumiza Timu ya Wananchi Hapa Tanzania yaani YANGA ..kwa nini kwa sababu ndiyo timu pekee kubwa na watu weusi kutoka kitongoji cha SOWETO KWA SASA Lakini pia kwa ambao tumeishi Afrika Kusini inapokutana Orlando Pirates na Kaizer Chief ni kama Umezikutanisha SIMBA (WAGENI Kaizer Chief) NA YANGA (WAZAWA Orlando Pirates)
Hii kwao ndiyo DERBY
(The Soweto derby between Kaizer Chiefs and Orlando Pirates is one of the most fiercely contested derbies in world football.)

Sababu nyingine ni kwamba Kaizer Chief ni Kama inatokea Mji wa Kishua (Johannesburg) ilihali Orlando Pirates Inatokea Uswazi (SOWETO)….JEZI ZA ORLANDO NI NYEUSI (WAAFRIKA HALISI) NA NYEUPE

The home jersey gives a strong nod to a club always respectful of its traditions, reimagining the iconic black colourway of Orlando Pirates

Kali kabisa inayofanya upinzai huu ni kwamba Kaizer Chief (1970 ilianzishwa na Msouth ambaye alikulia Marekani ilihali muasisi wa Orlando ni mzawa..KADHALIKA ukiitaja Orlando ni kama unaitaja timu ya wapiga kura kwani Kaizer Chief inajulikana kama TIMU YA VIONGOZI (Amakhosi )

Nembo ya OP ni fuvu lenye mifupa inayopishana na imeakisiwa kwenye FILAMU NYINGI ZA MAHARAMIA ila wenyewe LENGO LAO WANASEMA NI KUAMINI KATIKA NDUMBA ILI KUZITISHA TIMU PINZANI

Hii unayoisikia ya Mamelodi Sundowon (Kutoka Pretoria)ni KAMA AZAM TU YA HAPA, na inajaribu kuleta upinzani mkali kwa timu hizi mbili ….kwa sasa ndiyo inayoongoza LIGI KUU nchini SA

Orlando Pirates ina Uwanja wake wa Kisasa kabisa wenye uwezo wa kuingiza watu 40,000 na unaweza kupata picha MECHI YA MARUDIANO YA SIMBA…

OP kwa sasa inashikilia nafasi ya TANO kwenye msismamo wa Ligi Kuu ikiwa imecheza mechi 25, kushinda 9 na kufungwa mechi 4

Wachezaji hatari sana wa kuchungwa ni

  1. ABEL MABASO (Kiungo PUNDA)
  2. KABELO DIAMINI (Winga TELEZA)
  3. Tshegofatso Mabasa (Mshambuliaji Bull dozer)
    4 Paseka Mako-Beki Mshambuliaji
  4. Linda Mntambo (Kiungo mnyumbufu)

KILA LA HERI MNYAMA

Jumapili ya kihistoria, Kila la heri Simba SC.
Mtoto aliyeuwawa na mama yake alionesha mapema uoga wa kuishi nyumba hiyo