Jarida la Fobes linalochapishwa nchini Marekani limetoa orodha ya watu kumi wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani, huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Rais wa China, Xi Jinping ambaye ndiye mtu mwenye ushawishi mkubwa duniani kwa mujibu wa jarida hilo.

Xi Jinping amechukua nafasi hiyo mara baada ya bunge la nchi hiyo kupiga kura ya kumruhusu kuongoza kwa muda mrefu zaidi, akimpiku Vladmir Putin aliyekuwa akiishikilia nafasi ya kwanza.

Aidha katika nafasi ya pili ya watu wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani imechukuliwa na Rais wa Urusi, Vladmir Putin mara baada ya kuchaguliwa kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa nne mfululizo.

Rais wa Marekani, Donald Trump ameporomoka mpaka nafasi ya tatu mara baada ya kukumbwa na kashfa mbalimbali tangu aingie madarakani.

Nafasi ya Nne imechukuliwa na mwana mama ambaye inasemekana kuwa ndiye mwenye ushawishi mkubwa zaidi duniani, huyu ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye naye mwaka 2017 alishinda muhula wa nne kuiongoza nchi hiyo.

Mkuu wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos ameshika nafasi ya Tano katika orodha hiyo ya watu wenye ushawishi mkubwa duniani na ndiye mtu tajiri zaidi duniani kwasasa, anamiliki asilimia 16 za hisa za kampuni ya Amazon.

Papa Francis kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani anashika nafasi ya sita katika orodha ya watu wenye ushawishi mkubwa duniani, ni kiongozi wa kidini ambapo inakadiriwa kuwa anaongoza karibu waumini bilioni 1.2 wa dhehebu hilo

Nafasi ya Saba imechukuliwa na Bill Gates mwanzilishi wa Microsoft ambaye aliuza sehemu kubwa ya hisa zake lakini bado yuko kwenye bodi ya wakurugenzi.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman Al Saud ameshika nafasi ya Nane kwenye ordha hiyo wa watu wenye ushawishi mkubwa duniani, ambapo mwaka 2017 aliongoza kampeni ya kuwa kamatwa mafisadi wakubwa walikuwa wamejilimbikizia mali nchini Saud Arabia.

Nafasi ya Tisa imechukuliwa na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, na ndiye kiongozi wa pili kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao wa Twitter ambapo anawafuasi mil. 43 akiwa nyuma ya Rais Trump ambaye anaongoza kwakuwa na wafuasi wengi duniani kwa upande wa Twitter.

Nafasi ya Kumi iashikiliwa na Larry Page ambaye ni bilionea mwenza wa Google iliyoanzishwa kama mradi wa wanafunzi mwaka 1998 naye ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa duniani

 

 

 

 

 

 

Video: Kamanda Mambosasa amshukuru 'Mange' kurudi kundini
Usifanyie hiki mshahara wako