Wafanyabiashara katika Soko Kuu Mjini Tarime Mkoani Mara wamepokea mradi wa ujenzi wa soko kuu jipya utakao gharimu zaidi ya bilioni 8 fedha zilizotolewa na Serikali kuu ili kufanikisha ujenzi wa soko la kisasa.
 
Akizungumza na Wafanyabiashara wa soko hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Elias Ntiruhungwa amesema kuwa baada ya kupokea fedha hizo tayari halmashauri imetangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo.
 
Amesema kuwa vyanzo vingi vya mapato vilichukuliwa na Serikali kuu na halmashauri hiyo haina vyanzo vya uhakika vya mapato zaidi ya kutegemea mapato ya Soko hilo.
 
“Tunaishukuru Serikali imetupatia fedha baada ya kukidhi vigezo tukiwa miongoni mwa Halmashauri 12 tulioshinda kupata fedha za miradi na sisi ndiyo tumepata pesa nyingi na kwa mkoa wa Mara halmashauri yetu ya mji ndiyo tulioshinda na kupata fedha za miradi,”amesema Ntiruhungwa
 
Aidha, amesema kuwa vibanda vyote vilivyopo sokoni vitabomolewa hivyo Wafanyabiashara watatakiwa kuuza bidhaa zao kwenye maduka yaliyopo kwenye uwanja wa mpira, Soko la Rebu na maeneo mengine yenye vibanda.
 
Kwa upande wao, Wafanyabiashara wameunga mkono kwa kusema kuwa ujenzi wa soko jipya utakuwa ni mkombozi kwa usalama wa bidhaa zao kwani soko lililopo sasa limechakaa na miundo mbinu yake sio salama.
 
  • RC Ole Sendeka atajwa mkoani Njombe
 
  • Majaliwa amtumbua Mweka Hazina Kibondo
 
  • Kangi Lugola amng’oa mkuu wa kituo cha Polisi Mang’ola
 
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Sabasaba kupitia Chadema, Hamis Nyanswi amewataka Madiwani na Wanasiasa kuupokea mradi huo na wala kusiwepo pingamizi lolote kwakuwa fedha hizo zimetolewa na Serikali na si chama cha CCM wala Chadema

Benki ya Standard Chartered yaja na huduma mpya ya Kidijitali
Video: Timaya aachia ‘Balance’ kutoka kwenye albam yake mpya