Wafanyabiashara wa viumbe pori hai wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kufungulia biashara ya viumbe hao kutokana na kusitishwa mwezi Machi mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Viumbe pori hai  Salim Mussa,na kuongeza  kuwa wanamuomba Rais Magufuli aingilie kati suala hilo na kupata ufumbuzi wa kudumu wa kuendelea na biashara hiyo kwaajili ya kujiletea maendeleo yao na uchumi wa taifa kwa ujumla.

“Tunamuomba  Rais Magufuli aingilie kati suala hili na kutupatia ufumbuzi wa kudumu ili tuendelea na biashara ya viumbe pori hai bila ya usumbufu wa mara kwa mara kwani biashara hii ipo kwa mujibu wa sheria , taratibu na kanuni za nchi” alisema Salim.

Aidha  Salim amesema kuwa maamuzi hayo yanaweza kusababisha hasara kubwa kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa viumbe hivyo na uchumi wa nchi kwa ujumla kwani  muongozo haujatolewa tangu kusitishwa kwa biashara hiyo mwezi machi mwaka huu.

Kwa upande wake Msemaji wa wafanyabiashara hao Enock Balilemwa amesema kuwa kusitishwa kwa biashara hiyo kumepunguza kiwango cha ajira kwa kiasi cha watanzania milioni moja ambao asilimia 95 wanaishi vijijini.

Biashara hiyo ya viumbe pori hai inayojumuisha Vyura, wadudu, ndege,mijusi, tumbili, na mashamba ya wanyapori ilianza kabla ya uhuru sambamba na leseni zingine za uwindaji wa kitalii ambayo mpaka sasa inatambulika kwa sheria namba 5 ya mwaka 2009.

Majaliwa apokea msaada kutoa kwa Balozi wa Kuwait
Exclusive: Mwanzilishi wa MTV Africa afunguka mpango wa tuzo za MTV kufanyika Dar