Kufuatia Wafanyabishara wa Soko Matola lililopo Jijini Mbeya, kuwasilisha malalamiko yao kwa Serikali juu ya kutokuwepo kwa Uongozi rasmi katika Soko hilo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa ameagiza ndani ya mwezi mmoja uchaguzi uwe umefanyika.

Wakizungumza mara baada ya ziara ya Mkuu huyo wa Wilaya kutembelea sokoni hapo, walisema kwa muda mrefu soko hilo limekosa Viongozi sahihi na Viongozi waliopo hawapo kisheria kwani hawakuchaguliwa.

Katika maelekezo yake, Malisa alisema katika uchaguzi huo, wapatikane Viongozi watakaoweza kutetea maslahi ya Wafanyabishara hao.

Malisa amefanya ziara hiyo akianzia kata ya Iziwa ambapo alikagua shule ya Sekandari Iziwa na Kufanya mkutano wa Hadhara.

Meli ya msaada wa Mbolea yatia nanga Bandarini
Aliyeteseswa na mapenzi adai kupata tulizo la moyo wakeÂ