Wafanyakazi wa nyumbani jijini Nairobi wameandamana wakiomba Serikali kuwatambua kama wafanyakazi wengine ili waweze kupata manufaa ya ajira kama vile bima ya afya, likizo za uzazi na malipo ya uzeeni.

Wamesema mara nyingi wanapokuwa wagonjwa, jambo la kwanza mwajiri anafikiria ni kumfukuza.

“wafanyakazi wa nyumbani wamekuwa wakifutwa kazi kwa sababu ya ugonjwa, kila siku tunashugulikia kesi za aina hii” Amesema Khakame.

Hivyo wamesema wanapokuwa wagonjwa wana haki ya kulipwa kikamilifu siku saba za likizo.

Likizo yao ya kila mwaka haipaswi kuwa chini ya siku 21.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Wafanyakazi wa nyumbani, Ruth Khakame amesema Kisheria, waajiri wanatakiwa kuchangia malipo ya bima ya afya na hazina ya malipo ya uzeeni.

Aidha Kwa mujibu wa shirika na Kituo Cha Sheria, wafanyakazi wa nyumbani ni miongoni mwa makundi yanayokumbwa na changamoto zaidi.

Muungano wa wafanyakazi wa nyumbani, ambao umesajili zaidi ya wafanyakazi wa nyumbani 16,000, umekuwa ukiandaa vikao mara kwa mara kusikiliza malalamishi na kuwahamasisha wanachama

Kwa mujibu wa Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) asilimia 30 ya wafanyakazi wa nyumbani huwa ni watoto.

Wanawake wanajumuisha asilimia kubwa na Kenya peke yake ina wafanyakazi wa nyumbani zaidi ya milioni 2.

 

21 wahukumiwa kifo, kiongozi wa dini abariki
Utafiti wazitaja nchi zinazoongoza kwa rushwa sekta ya umma