Wachimbaji madini watatu wamefariki kwa kukosa hewa baada ya kuchoma dawa za kienyeji walizopewa na mganga wa kienyeji wakiwa chini ya mgodi kwa lengo la kupata madini mengi.

Akizungumza jana mjini Bukoba kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, Revocatus Milami, amewataja wachimbaji hao ambao ni araia wa Burundi, Sinzumusi Gerald (28), Minani Ramadhani (47) na Muhambazi Severen (50).

Amesema tukio hilo lilitokea Desemba 17, mwaka huu ambapo wachimbaji hao na mwingine mmoja aliyefanikiwa kutoroka walikuwa wakichimba madini aina ya Orphram na Tantlite katika kitongoji cha Murogomero kijiji cha Kihanga mkoani Kagera.

“Katika tukio hilo wachimbaji walikuwa wanne ambao walipewa sharti na mganga wa kienyeji kuwa wakachome moto dawa ndani ya mgodi huo uliokuwa na kina cha mita 30 ili wanuize kwaajili ya kupata madini mengi” alisema kamanda Malimi.

Na kuongeza “Baada ya kuchoma dawa hiyo wachimbaji hao walikosa hewa ambapo wawili walifanikiwa kutoka na mmoja akatoroka lakini mmoja alienda kutoa taarifa kwa serikali za mitaa”.

Kiwanda cha nyama ya Punda chaadhibiwa uchafuzi wa Mazingira
Video: Uteuzi wa Mnyika watikisa, Kigogo mwingine aunganishwa kesi ya Sethi, Rugemalira