Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni wapenzi wamefariki dunia mkoani Njombe baada ya kuweka jiko la mkaa katika chumba walichokuwa wanalala ili kupunguza ukali wa baridi.

Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani Njombe Hamis Issa, amesema watu hao waliofahamika kwa jina la Benitho Mbata  ambaye ni mkazi wa national Housing mjini Njombe na Jazira Said Mkazi wa Namtumbo wamefariki dunia kutokana na gesi hatari ya mkaa.

Aidha Kamanda Issa amewataka wananchi kutafuta njia za kukabiliana na baridi ikiwemo kuvaa mavazi mazito badala ya kukoleza mkaa na kisha kuweka jiko vyumbani.

Katika tukio jingine Kamanda Issa amesema mtu mmoja kafariki dunia baada ya kudondokewa na mti ambao alikuwa akiukata mwenyewe, na kisha kutoa rai kwa watu wanaohitaji kukata miti kuhitaji ushauri wa kitalaamu ili kunusuru maisha yao.

Amesema Katika Mkoa wa Njombe kuanzia mwezi June hadi Septemba huwa ni kipindi cha baridi kali hivyo matumizi ya mkaa huongezeka.

Madaraja kurekebishwa nchi nzima
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 22, 2021