Zaidi ya wafilipino zaidi ya 1000 wameandamana mjini Manila dhidi ya mpango wa kuuzika mwili wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Ferdinand Marcos, kwenye eneo la mashujaa wa taifa hilo.

Waandamanaji hao walihimili mvua kubwa iliokuwa ikinyesha, na kumuomba rais wa sasa , Rodrigo Duterte, kufuta mpango huo.

Mwaandamanaji mmoja, seneta Risa Hontiveros, amemtaja rais Duterte kuwa adui wa mashujaa wa Ufilipino.

Rais huyo wa awali anatuhumiwa kuhusika katika ufisadi , na ukiukaji wa haki za binaadamu.

Serikali yake ilipinduliwa mwaka wa 1986, na aliaga dunia akiwa uhamishoni miaka mitatu baadaye

Imamu Na Msaidizi Wake Wauwawa New York
Chadema Yabwagwa Kesi Ya Maandamano,Yakosa Hoja Za msingi za Kutetea Maandamano, Serikali Yaibuka Kidedea