Wafuasi 12 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa madai ya kumshambulia mgombea wa nafasi ya diwani kutoka Chama cha Mapinduzi CCM.

Polisi pia wamekamata gari la matangazo linalotumiwa na chama hicho kutangaza mikutano mbalimbali katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Muriet hivyo kuwasababishia wanachama wa chama hicho kutopata taarifa za mikutano.

Aidha, Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amesema kuwa wafuasi hao wa chadema walikamatwa juzi usiku katika eneo la la FFU kwa Morombo ambapo wanakabiliwa na tuhuma za kufanya shambulizi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa watuhumiwa hao waliwavamia wafuasi wa CCM wakati wakitoka katika mikutano ya kampeni katika eneo la Muriet na kuanza kuwashambulia bila kosa lolote.

Manchester City kuweka rekodi hii ikiwafunga Arsenal
Kante kuibeba Chelsea leo?