Wafuasi watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na raia wa kigeni watatu wamefutiwa kesi ya kuingilia utangazaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana, iliyokuwa ikiwakabili.

Jana, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam iliamua kufuta kesi hiyo baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuiambia mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kesi hiyo imefutwa wakati ikiwa katika hatua za awali za kusikilizwa baada ya upande wa wa mashtaka kueleza hapo awali kuwa umekamilisha ushahidi dhidi ya washtakiwa hao.

Washtakiwa hao ambao ni Mashinda Mtei, Julius Mwita, Fredrick Fussi, Meshack Mlawa na Anisa Rulanyaga, raia wa Tanzania. Raia wa kigeni ni Julius matei (Mkenya), Jose Nimi wa Angola (hivi sasa ni marehemu), Kim Hyunwook (Korea).

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa Mahakamani hapo, ilidaiwa kuwa watuhumiwa kwa pamoja, kati ya Oktoba 25 na 26 mwaka jana walichapisha na kusambaza matokeo ya uchaguzi ambayo hayakuthibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kinyume cha sheria ya makosa ya mtandao namba 14 ya mwaka 2015.

Serikali kumalizana na Dangote
Video: Eric Omondi alivyoifanya 'Kuliko Jana' ya Sauti Sol