Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Karatu, Thomas Darabe, amepandishwa kizimbani na wenzake saba,katika Mahakama ya Wilaya Arumeru kwa kosa la uharibifu wa mali zenye thamani ya zaidi ya milioni 73.

Darabe ambaye pia ni Diwani wa kata ya Barai Wilayani humo amefikishwa mahakamani hapo pamoja na Diwani wa kata ya Mangiola, Lazaro Emmanuel(CCM),na Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumiaji maji Mangiola, Charles Lameck.

Katika kesi hiyo ya jinai namba tatu ya mwaka 2017,Mwendesha mashtaka wa Serikali, Adelina Kassalla amedai kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo kwa makusudi kinyume na kifungu cha 326(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Aidha, watuhumiwa hao waliharibu injini aina ya Massey,yenye thamani ya shil.milioni12, pampu ya maji yenye thamani ya sh. 3,000,000 mali ya Daniel awaki, mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC).

Hata hivyo kesi zote zimeahirishwa hadi januari 16 mwaka huu ambapo zitatajwa tena kutokana na upelelezi wa mashauri hayo kutokamilika.

Take one kurudi tena hewani
Dk. Mongela ahofia kasi ya JPM

Comments

comments