Mzimu wa kupigana ngumi mahakamani kati ya wafuasi wa CUF wanaomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na wale wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad umeibuka tena leo Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Ikiwa ni mara ya pili kwa wafuasi hao kupigana ngumi mahakamani hapo, leo ugomvi huo umewahusisha walinzi wa pande hizo mbili ambao wanafahamika kama ‘Mabaunsa’.

Wafuasi hao walijikuta wakishindwa kuvumiliana kwa mara ya pili walipofika kusikiliza uamuzi wa Mahakama kuhusu shauri la Maalim Seif kupinga Jaji Sekieti Kihiyo kusikiliza kesi hiyo kwa madai kuwa hana imani naye.

Jeshi la polisi liliingia ugomvi huo wa walinzi na kufanikiwa kuuzima muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Awali, wafuasi wa CUF wa pande mbili walipigana Makonde mahakamani hapo katika siku ya kwanza kwa pande hizo kufika mahakamani kusikiliza kesi ya msingi ambapo Baraza Kuu la chama hicho limeiomba Mahakama hiyo kubatilisha barua ya Msajili wa vyama vya siasa ya kumtambua Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa chama hicho na pia kuiomba imzuie Msajili kuingilia maamuzi ya ndani ya chama.

Baraza Kuu la CUF lilimvua uanachama Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na viongozi wengine waliodaiwa kuhusika kukihujumu chama hicho, uamuzi ambao msomi huyo amedai ni batili.

Chadema watoa tamko kuhusu kupotea kwa msaidizi wa Mbowe
Kotei,Luizio Wasajiliwa Msimbazi, Vincent Angban Atemwa