Chama kipya cha siasa kilichoanzishwa wiki iliyopita nchini Zimbabwe kimeonesha mwanga wa kuwa chama cha vigogo wa Zanu-PF ambao bado ni watiifu kwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe.

Mapema wiki hii, mmoja kati ya wa viongozi wa Zanu-PF aliyewahi kuhudumu kama waziri kwenye serikali ya Mugabe, Ambrose Mutinhiri alitangaza kujiengua na chama hicho tawala na kujiunga na chama hicho kipya kinachoitwa ‘New Patriotic Front (NPF)’.

Gazeti la Standard la nchini humo limemkariri Mutinhiri akieleza kuwa amechukua uamuzi huo kwakuwa hakubaliani na kitendo cha jeshi kuingilia masuala ya kisiasa na kumuondoa Mugabe.

“Kuelekeza mitutu ya bunduki kwa Mugabe ilikuwa ni sawa na kuelekeza mitutu ya bunduki na makombora ya kijeshi kwa mamilioni ya wananchi ambao walimpigia kura kumuweka madarakani,” alisema Mutinhiri.

Taarifa zilizotokana na vyanzo vya gazeti hilo zimeeleza kuwa Mutinhiri alikutana na Mugabe na mkewe Grace nyumbani kwao jijini Harare wiki iliyopita na kwamba alikabidhiwa jukumu la kuongoza chama hicho kipya cha NPF.

Aiba tuzo ya Oscar ya Muigizaji bora wa kike, polisi wapambana
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 6, 2018