Wafugaji wawili wamezuiliwa katika kituo cha kurekebisha tabia kwa kupatikana na hatia ya kumteka nyara na kumbaka mwanamke mmoja mjamzito (jina linahifadhiwa), katika eneo la Federal Capital Territory, jiji Abuja nchini Nigeria.

Mwendesha mashitaka wa Mahakama, Dabo Yakubu ameiambia Mahakama ya Gwagwalada kuwa washtakiwa Nuru Tukur (21), na Yusufa Haruna (29), Februari 25, 2023 walimteka na kumbaka mama mjamzito wa miezi minane katika nyumba yake iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Abaji ya FCT.

Mkunga, Sieneh Borbor (42), akimchunguza mjamzito Emma Vah ( 40), kabla ya kupokea matibabu ya kuzuia malaria Kliniki ya Careysburg katika Kaunti ya Montserrado, Liberia Aprili 13, 2021. Picha ya The Star.

Amesema, wafuwafugaji hao walimpeleka mhasiriwa porini ambapo wote wawili walimbaka bila kujali kwamba alikuwa na ujauzito wa miezi minane, ambapo Wakili wa Halmashauri ya Eneo la Abaji, Abubakar Obina akiripoti suala hilo ofisi ya Kamandi Gwagwalada siku moja baadaye

Mwendesha mashtaka huyo, Yakubu ameongeza kuwa, makosa hayo yanakiuka Kifungu cha 96, 262, 264, 387 cha Kanuni ya Adhabu na Hakimu, Malam Abdullahi Abdulkarim, aliahirisha hukumu, ili aweze kuona na kujua hali ya mwathiriwa.

Tanzania, Namibia kuimarisha Diplomasia ya Uchumi
Mbowe alinanga kundi la kina mdee mbele ya Rais Samia