Wafugaji Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora, wametishia kugoma ili kushinikiza Halmashauri ya wilaya hiyo  kuwatengea  maeneo ya malisho ili kukomesha kamata kamata ya mifugo, vipigo, dhuluma na faini za mamilioni ya fedha wanazotozwa kila kukicha  kutoka kwa Maofisa Maliasili.

Hayo yamesemwa a viongozi wa wafugaji hao, walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari wilayani humo.

Aidha, Wafugaji hao wameiomba Serikali kupitia Halmashauri hiyo imalize kilio chao kwa kuwapatia maeneo ya kutosha ya kulishia mifugo yao kwakuwa eneo lilipo kwa sasa linatumika kwa makazi na kilimo, huku eneo lililopo la ufugaji ni asilimia tano tu, wakati asilimia 95 ni eneo la wazi na hifadhi ya mbuga.

Kwa upande wake Katibu wa Wafugaji Wilaya ya Sikonge, Nyenge Lusondagula, amesema kuwa wako tayari kugoma ili kuishinikiza Serikali iwaonee huruma, kwani kukosekana kwa maeneo ya malisho na maji yana athiri ubora wa mifugo yao.

“Inasikitisha sana kuona wafugaji wananyanyaswa na kuteswa na kudhalilishwa kila siku wakati Mifugo ni rasilimali inayohitajika ndani na nje ya nchi na inachangia sana pato la taifa na kukuza uchumi wa wafugaji”amesema Lusondagula.

 

Yanga kuinyemelea Simba leo? Lwandamina afanya yake
Machinga wageuka ‘pasua kichwa’ Morogoro