Kundi la wafugaji limevamia eneo la wakulima na kuua watu watano katika eneo linalowakutanisha wakulima na wafugaji pembeni mwa jijini la Lagos nchini Nigeria.

Mauaji hayo yanatokana na mgogoro uliopo kuhusu haki ya malisho na kulima katike eneo hilo.

Jeshi la polisi limeeleza kuwa tukio hilo limetokea jana na kwamba mbali na mauaji hayo, watu hao wenye silaha pia waliwajeruhi makumi ya wakulima.

Tukio hilo limetokea wakati ambapo Rais Muhammadu Buhari anamalizia ziara yake katika maeneo ya karibu na moja kati ya mambo anayofanya ni kuhamasisha utulivu kati ya makundi hayo mawili.

“Watu wenye bunduki ambao wanaaminika kuwa ni wafugaji walivamia na kuwashambulia wakaazi wa wilaya ya Miango na kuua watu watano,” msemaji wa polisi, Terna Tyopev aliiambia AFP.

Aidha, alisema wavamizi hao waliharibu makaazi, mashamba na mali nyingine za wakulima. Jeshi hilo linawasaka wavamizi hao ili wafikishwe kwenye mikono ya sheria.

Lissu kufanyiwa upasuaji wa 19, atuma ujumbe
Nikki wa Pili awabana BASATA na nyimbo chafu wakati wa uchaguzi