Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imethibitisha maambukizi ya virusi vya Corona kwa wafungwa wapatao 100 katika gereza la kijeshi mjini Kinshasa.

Taarifa ya hivi karibuni kutoka wizara ya Afya mjini Kinshasa inasema kuwa visa 101 vya COVID-19 vimethibitishwa katika gereza hilo la kijeshi, ingawa 92 kati ya walioambukizwa walikuwa katika hali nzuri.

Kumbukumbu za kikao cha baraza la mawaziri ambazo nakala yake imeonekana na shirika la habari la AFP, zimesema maambukizo hayo yanaweza kuwa kitisho kikubwa kwa jamii, hususan ikiwa yataenea hadi gereza la Makala lenye msongamano mkubwa wa wafungwa.

Kumbukumbu hizo zimesema kwa kuzingatia jinsi maambukizi yalivyosambaa kwa kasi katika gereza la kijeshi la Ndolo, uwezekano wa kulifikia gereza la Makala hauwezi kupuuzwa. 

Mtoto wa miezi 6 aambukizwa corona, visa vyaongezeka Kenya
AU kuchunguza dawa ya Corona kutoka Madagascar