Watu wawili wamefungwa jela baada ya kumchezea vibaya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza katika mchezo wa mpira wa miguu uliomshirikisha Rais huyo.

Rais Nkurunziza anapenda kusafiri na Timu yake ya mpira wa miguu ya Haleluya FC pamoja na Kwaya iitwayo “Komeza Gusenga” ya kanisa la Evangelical Christian ambalo huwa anapenda kusali.

Timu ya Rais Nkurunziza ilikuwa ikicheza na timu nyingine kutoka Kaskazini mwa nchi hiyo katika Mji wa Kiremba.

Katika mchezo huo uliowajumuisha wakimbizi wa kutoka Congo ambao hawakufahamu kama Rais Nkurunziza pia ni miongoni mwa mchezaji ambao hao ndio walimchezea rafu.

Mara nyingi Rais Nkurunziza anapocheza katika michezo ya kirafiki wapinzani wake humpatia nafasi ya upendeleo na kumuache atawale na hata kufunga magoli lakini katika mchezo huo haikuwa hivyo.


Ukimkuta mpenzi wako ana “RED BLOOD CELLS” utafanyaje? | Penyenye za Kitaa (S01E01)

TMA yatoa tahadhari kwa wananchi
Simba SC yatangaza viingilio dhidi ya Al Masry