Kiungo kutoka nchini Brazil, Ricardo Izecson dos Santos Leite (Kaka), amatajwa kuwa mchezaji anaelipwa pesa nyingi miongoni mwa wachezaji wanaocheza ligi ya nchini Marekani kwa sasa.

Uchunguzi uliofanywa na umoja wa wachezaji wa ligi hiyo (MLS) umebaini Kaka ameingiza kiasi kikubwa cha pesa kwa mwaka 2016 na kufikia dola za kimerekani milioni 7.167 sawa na Pauni milioni 4.92.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34, ametajwa kuwa kinara kwa kujikusanyia pesa nyingi kwa mwaka wa pili mfululizo, akifuatiwa na mshambuliaji kutoka nchini Italia, Sebastian Giovinco aliyejikusanyia kiasi cha dola za Marekani milioni 7.115.

Ripoti ya uchunguzi huo imefafanua kwamba, pesa hizo zimejumuisha mapato ya mishahara pekee kwa wachezaji ambao orodha yake imetolewa mapema hii leo.

Hata hivyo wachezaji wa kigeni wameonekana kuwa katika malipo ya juu, tofauti na ilivyo kwa wazawa, ambapo idadi yao ni hafifu kwenye orodha ya wachezaji kumi bora.

Nahodha wa timu ya taifa ya Marekani Michael Bradley ametokea katika orodha hiyo kwa kuonekana kuwa mzawa anaelipwa pesa nyingi, ambapo amejikusanyia kiasi cha dola milioni 6.5 (Pauni Milioni 4.46), akifuatiwa wachezaji wengine wakigeni kutoka nchini England, Steven Gerrard na Frank Lampard.

Orodha ya wachezaji kumi bora waliojikusanyia pesa nyingi kutokana na mishahara yao kwa mwaka 2016.

Kaka (Orlando City) – $7.167 million (£4.92 million)

Sebastian Giovinco (Toronto FC) – $7.115 million (£4.88 million)

Michael Bradley (Toronto FC) – $6.5 million (£4.46 million)

Steven Gerrard (Los Angles Galaxy) – $6.132 million (£4.21 million)

Frank Lampard (New York City FC) – $6.0 million (£4.12 million)

Andrea Pirlo (New York City FC) – $5.915 million (£4.06 million)

David Villa (New York City FC) – $5.610 million (£3.85 million)

Jozy Altidore (Toronto FC) – $4.825 million (£3.31 million)

Clint Dempsey (Seattle Sounders) – $4.605 million (£3.16 million)

Giovani Dos Santos (Los Angeles Galaxy) -$4.25 million (£ 2.92 million)

Video: Manny Pacquiao ashinda Useneta, Atajwa kuwa Rais wa Ufilipino ajaye
Enner Valencia Kuwarithi Victor Anichebe, Stephane Sessegnon