Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil Neymar da Silva Santos Júnior alikataa kujiunga na mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain, wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.

Mmiliki wa Paris Saint-Germain Nasser Al-Khelaifi, aliamua kulivalia njua suala la usajili wa mshambuliaji huyo lakini alishindwa kutokana na msimamo uliokua umewekwa na mshambuliaji huyo, ambaye ni mchezaji halali wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona.

Wakala wa Neymar (Wagner Ribeiro) amefichua siri hiyo na kuianika baada ya kufanya mazungumzo na ESPN Brazil, ambapo amesema Al-Khelaifi alimuahidi mchezaji wake mshahara wa Pauni laki sita na nusu (650,0000) kwa juma pamoja na ndege binafsi lakini bado lengo lake halikufanikiwa.

Ribeiro ameendelea kubainisha kuwa, mbali na ofa hiyo kwa Neymar, kibopa huyo kutoka falme za kiarabu alikua ametenga kiasi cha Pauni milioni 160 kama ada ya usajili.

Ribeiro amesema “Tumewahi kukutana na kufanya mazungumzo na Nasser [Al-Khelaifi] kuhusu suala la uhamisho wa Neymar, lakini mara zote mambo yalikua yanakwenda tofauti na alivyotarajia, kutokana na muhusika kuonyesha nia ya kubaki Camp Nou.

“Nilijaribu kumwambia Neymar juu ya ofa hiyo ambayo ni vigumu kwa mtu yoyote kuipa kisogo… lakini alikata kata kata.”

UEFA Wapata Rais Mpya, Kuongoza Hadi 2019
Moutinho Aeleza Alivyoshindwa Kujiunga Na Spurs