Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Arumeru Mashariki, Emmanuel Mkongo amebainisha sababu ya aliyekuwa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Palangyo kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki, ni kwamba baadhi ya wagombea kutorudisha fomu za kuwania ubunge.

Ameyasema hayo wakati akitangaza sababu ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupita bila kupingwa, ambapo Mkongo amesema kuwa idadi kubwa ya wagombea walishindwa kufuata taratibu na sheria zinazoongoza kanuni za Uchaguzi wa Urais, Ubunge na Udiwani.

Amesema kuwa wagombea watatu hawakuteuliwa kwasababu hawakurudisha fomu, ambao ni Antonia Ndosi (DP),George Nashoini (CUF) na Msifuni Mwanga (TLP), huku fomu za wagombea wengine saba zilirudishwa lakini zilikuwa na mapungufu ya kisheria.

“Mgombea wa SAU hakuteuliwa kwa sababu hakudhaminiwa na wapiga kura 25, na kushindwa kukidhi matakwa ya sheria ya uchaguzi, mgombea huyu pia hakulipa dhamana ya shilingi 50000.” amesema Mkongo

April 19, 2019 Msimamizi huyo wa Uchaguzi alimtangaza aliyekuwa Mgombea wa CCM Dkt. John Pallangyo kuwa Mbunge mteule wa Jimbo la Arumeru Mashariki na kurithi nafasi ya Joshua Nassari.

Baada ya kipigo, Manara amvaa Zahera, 'Unatakiwa ujifunze kuongea mnapofungwa'
Wananchi mkoani Njombe wamtosa kiongozi wao, 'Tatizo hapa ni siasa'

Comments

comments