Saa chache baada ya zoezi la kupiga na kuhesabu kura kukamilika katika maeneo mengi nchini, taa ya kijani kuelekea Dodoma imeanza kuonekana kwa baadhi ya wagombea ubunge ambao wamejitangaza kufuatia matokeo ya awali.
Baadhi ya wagombea wameyatumia matokeo ya awali yaliyotangazwa na kubandikwa katika vituo vya kupigia kura.
Mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ni mmoja kati ya wagombea waliojitangaza mapema jana jioni.
I dedicate this to my friend Deo Haule Filikunjombe. It is his victory and I won’t celebrate this as to me the election became meaningless
— DEO!KaziYaMungu (@zittokabwe) October 25, 2015Naye Peter Serukamba, Mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CCM alitangaza kupitia akaunti yake ya Twitter akiwashukuru wapiga kura wa jimbo la Kigoma Kaskazini.
Kigoma north have spoken, am deeply humbled!
— peter serukamba (@pjserukamba) October 25, 2015
Matokeo tunayoyapokea kutoka kwa mawakala wa CCM nchi nzima, yanaonyesha ushindi usio na shaka. https://t.co/RS40AS7CX5
— January Makamba (@JMakamba) October 25, 2015
Hata hivyo, matokeo ya awali yameanza kuonesha ishara nzuri kwa baadhi ya wagombea ubunge wa Ukawa waliotajwa kuwa wanaongoza ni pamoja na Ester Matiku (Tarime Mjini), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki).
Tundu Antiphas Mughwai Lissu akifurahia kuongoza katika kura za Ubunge jimbo la Singida Mashariki. #tanzaniadecides pic.twitter.com/bkliXqWRyr
— Uchaguzi Mkuu (@uchaguzimkuu) October 26, 2015
Majimbo ya Ilemela na Nyamagana jijini Mwanza yanaonekana CCM inaongoza ikiwa imechukua kata nyingi zaidi. Jimbo la Musoma Mjini linaonekana kuwa na dalili zote za kuwa mikononi mwa CCM hivi sasa kwani matokeo ya awali yanaonesha kata 14 kati ya 16 zimeshikiliwa na CCM.
NEC inatarajia kutanganza matokeo rasmi leo kuanzia saa tatu asubuhi na lolote linaweza kutokea kwani hayo ni matokeo ya awali.