Jina la rais John Magufuli limeendelea kuvuma kwa kasi katika nchi za bara la Afrika kutokana na utendaji wake wa kazi ndani ya kipindi kifupi tena bila kuwa na baraza la Mawaziri.

Kasi hiyo ya maendeleo na kubana matumizi imewafanya wagombea urais wa Uganda kuwaahidi wananchi wao kuwa endapo watamchaguliwa watafanya kazi kama rais Magufuli.

Anayeongoza kwa kulitaja jina la Magufuli kwenye kampeni zake ni Dk. Kizza Besigye ambaye ni mpinzani mkubwa wa rais Yoweri Mseveni kwenye kinyang’anyiro hicho cha urais.

Dk. Kizza Besigye

Dk. Kizza Besigye

Dk. Besigye anayewania urais kwa tiketi ya chama cha Forum for Democratic Change (DDC), amekuwa akiwaambia wananchi kwenye kampeni zake kuwa atakapoingia madarakani atafuata nyayo za Dk. Magufuli kwa kuanza kuuza ndege ya rais ambayo alisema inawabebesha mzigo walipa kodi.

Besigye alijinasibu kuwa atauza ndege hiyo yenye thamani ya shilingi za Tanzania bilioni 55.6 (sawwa na shilingi za Uganda bilioni 88.2), na kwamba fedha hizo atazitumia katika maendeleo ya jamii.

 

Quick Rocka amuweka hadharani Kajalla
Podolski Akutana Uso Kwa Macho Na Mayweather