Waziri wa Habari wa Zimbabwe, Monica Mutsvangwa amesema zaidi ya watoto 700 wamefariki kutokana na ugonjwa wa surua nchini uliozuka nchini humo katika mtukio lililoripotiwa kwa mara ya kwanza mwezi Aprili, baada ya Watoto wengi kutochanjwa kwa sababu za kiimani na kidini.

Akiongea na vyombo vya Habari, Waziri Mutsvangwa amesema Serikali ilitangaza mpango wa chanjo lakini, kama ilivyo kwa maradhi ya Uviko-19, baadhi ya vikundi vya kidini na kiimani vilipinga kwa ukaidi chanjo na kuzuia kampeni hiyo, huku baadhi yao wakiwapa watoto wao chanjo kwa siri.

Vikundi vya kitume vinavyoingiza imani za kimapokeo katika fundisho la Kipentekoste ni miongoni mwa vinavyotilia shaka dawa za kisasa nchini humo na wafuasi huweka imani yao katika sala, maji matakatifu na hatua zingine za kuzuia magonjwa au kuponya magonjwa.

Kumekuwa na utafiti mdogo wa kina kuhusu makanisa ya Kitume nchini Zimbabwe, lakini tafiti za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF), inakadiria kuwa ndilo dhehebu kubwa zaidi lenye wafuasi karibu milioni 2.5 katika nchi hiyo yenye watu milioni 15, na hata hivyo baadhi ya Makanisa yamekuwa yakiwaruhusu kupata huduma hiyo ya chanjo.

Waziri huyo ameongeza kuwa, “ili kuokoa watoto wao akina mama wengine hutembelea kliniki kwa siri, nyakati fulani usiku na bila waume zao kujua na kundi la waumini wa kanisa la Mitume ambao wako tayari kutumia dawa za kisasa wamekuwa wakijaribu kubadili mitazamo ya kanisa, lakini pia wanashauri wanawake kuwasaidia watoto wao.”

WHO na UNICEF, zinasema ongezeko la asilimia 79 ya surua katika miezi miwili ya kwanza ya 2022 pekee na kuonya juu ya uwezekano wa milipuko mikubwa na kwamba Watoto na wajawazito wako katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa surua, huku zaidi ya asilimia 95 ya vifo vya surua hutokea katika nchi zinazoendelea.

Kikosi cha Simba SC safarini Zanzibar
Djigui Diara atuma salaam kwa Mashabiki Young Africans