Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao wa Hospitali ya Meditrina ya nchini India wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa siku tatu ya kuzibua mishipa ya damu  ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa (Chronic Total Occlusion) na hivyo kushindwa kupitisha damu vizuri.

Kambi hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye matatizo hayo ambao bila ya kupata mtaalamu mwenye ujuzi wa hali ya juu wa kuzibua mishipa hiyo wangefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.

Aidha, matibabu hayo yanafanyika kwa kutumia mtambo wa Cathlab ambapo mgonjwa anatobolewa tundu dogo katika paja ambalo linapitishwa vifaa maalum vya kuzibua mishipa ya damu ya moyo (Stent).

Katika kambi hiyo wataalamu wa afya wa JKCI watapata elimu ya jinsi ya kuzibua mishipa ya damu ya moyo ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa.

Jumla ya wagonjwa 15 ambao mishipa yao ya damu mmoja hadi mitatu imeziba wanatarajiwa kutibiwa katika kambi hiyo iliyoanza leo tarehe 23 hadi  25/4/2019. hadi sasa wagonjwa watano wameshatibiwa na hali zao zinaendelea vizuri.

Kikwete aliendeleza mahusiano mazuri na IMF- Prof. Lipumba
TFF yaishushia rungu Yanga,