Wizara ya afya nchini Tanzania imetangaza visa vipya vya wagonjwa wa Corona, 14 ambavyo vimethibitishwa kutokea siku ya Aprili 13, 2020, ambao wote ni watanzania.

Katika taarifa iliyotolewa imeeleza kuwa wagonjwa hao 13 ni wakazi wa Dar es salaam na mmoja ni mkazi wa Arusha, na kwa ongezeko hilo imefanya wagonjwa kuwa 46 kutoka 32 ambao walitolewa taarifa awali Aprili 10, 2020.

Hii ni idadi kubwa ya visa kutangazwa kwa wakati mmoja, tokea kisa cha kwanza kilipotangazwa mwezi Machi mwaka huu.

Serikali imeendelea kusisitiza wananchi kuendea kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu kama elimu inavyotolewa mara kwa mara kupitia njia mbalimbali.

Corona yapunguza uzalishaji wa mafuta duniani
Video Mpya: Waite – Esaya Feat Jazz Bee #support